Mshindi wa pili wa shindano la Big Brother Africa Stargame,
Jackson Makini aka Prezzo amesema Mungu alikuwa na sababu yake kumfanya akamate
nafasi ya pili.
Amesema anaamini kuwa kwa nafasi hiyo kuna mengi mema yapo
njiani yanakuja kwaajili yake.
Akiongea na kipindi cha Amplifaya cha Clouds Fm, Prezzo
amechukua muda huo kuzungumzia pia taarifa ya gazeti la Daily Post la Kenya
lililodai kuwa atakuwa akilipwa dola 720,000 kwa mwaka kama balozi wa One Campaign.
Amesema ameshangaa kuona habari hiyo na kudai kuwa anatamani
ingekuwa kweli kwakuwa hakuna kitu kama hicho.
Msikilize zaidi hapa kwenye interview hiyo.
